TAASISI YA MO DEWJI YATUNUKIWA TUZO YA UBORA YA SUPERBRANDS "Credit News 24" | Credit News 24

TAASISI YA MO DEWJI YATUNUKIWA TUZO YA UBORA YA SUPERBRANDS "Credit News 24"

About TAASISI YA MO DEWJI YATUNUKIWA TUZO YA UBORA YA SUPERBRANDS "Credit News 24" - Credit News 24, we has prepared this article well for you to read and retrieve information in it. Okay, happy reading.

TAASISI YA MO DEWJI YATUNUKIWA TUZO YA UBORA YA SUPERBRANDS "Credit News 24"

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo ya ubora ya Superbrands.

Tuzo ya Superbrands ambayo Taasisi ya MO Dewji imetunukiwa.
Taasisi ya MO Dewji inayojihusisha na kusaidia jamii katika elimu, afya na maendeleo ya jamii imetunukiwa tuzo ya kimataifa ya ubora inayofahamika kama Superbrands.

Taasisi hiyo inayomilikiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mohammed Entreprises Tanzania Limited, Mohammed Dewji imetunukiwa tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali ambayo inaifanya.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez amesema ni heshima kubwa kwa taasisi kupata tuzo hiyo lakini pia itawasaidia kufanikisha miradi mikubwa ambayo wamepanga kuifanya na taasisi kubwa kama ya Bill Gates.

“Kwa niaba ya Taasisi ya MO Dewji na kampuni ya MeTL Group tunashukuru sana kwa tuzo hii na huu ni mwanzo mpya wa safari yetu, kama mnavyojua taasisi yetu ilianzishwa mwaka 2014 na katika kipindi cha miaka miwili tumeanzisha miradi mbalimbali kama MO Entrepreneurs na MO Scholars ikiwa na lengo la kuwasaida vijana na tunafuraha Baraza la Superbrands limetutambua,

“Tuzo hii inatusaidia katika miradi mikubwa kwa sasa kama taasisi ya Mohammed Dewji tunataka kufanya ushirikiano na taasisi kubwa kama Taasisi ya Bill Gates, kushirikiana na taasisi za Kenya, Uganda, UK, jina la Mohammed Dewji litakuwa la kwanza na SuperBrand litakuwa ya pili,” amesema Barbara.

This is the article TAASISI YA MO DEWJI YATUNUKIWA TUZO YA UBORA YA SUPERBRANDS "Credit News 24" this time, hopefully can benefit for you all. well, see you in other article post.

Title : TAASISI YA MO DEWJI YATUNUKIWA TUZO YA UBORA YA SUPERBRANDS "Credit News 24"
link : TAASISI YA MO DEWJI YATUNUKIWA TUZO YA UBORA YA SUPERBRANDS "Credit News 24"

0 Response to "TAASISI YA MO DEWJI YATUNUKIWA TUZO YA UBORA YA SUPERBRANDS "Credit News 24""

Post a Comment