MATOKEO YA UUZWAJI WA HISA 560,000,100 ZA VODACOM TANZANIA KATIKA SOKO LA AWALI "Credit News 24" | Credit News 24

MATOKEO YA UUZWAJI WA HISA 560,000,100 ZA VODACOM TANZANIA KATIKA SOKO LA AWALI "Credit News 24"

About MATOKEO YA UUZWAJI WA HISA 560,000,100 ZA VODACOM TANZANIA KATIKA SOKO LA AWALI "Credit News 24" - Credit News 24, we has prepared this article well for you to read and retrieve information in it. Okay, happy reading.

MATOKEO YA UUZWAJI WA HISA 560,000,100 ZA VODACOM TANZANIA KATIKA SOKO LA AWALI "Credit News 24"


Toleo la hisa za Kawaida za Kampuni ya Vodacom Tanzania Public Limited Company (“Vodacom Tanzania” au “VODA”) kwa bei ya TZS 850/= kila hisa lilizinduliwa Alhamisi tarehe 9 Machi, 2017 na kuhitimishwa Ijumaa tarehe 28 Julai, 2017. Toleo lilenga kukusanya jumla ya TZS 476,000,085,000 kutokana na mauzo ya hisa 560,000,100.

Matokeo ya toleo hilo yanaonyesha kuwa kiasi cha TZS 476,000,085,000 kilikusanywa kama ilivyopangwa. Kati ya mauzo hayo, 60% imeotokana na mauzo kwa wawekezaji wa hapa Nchini na 40% imetokana na mauzo kutoka kwa waekezaji wa Kimataifa.

Taarifa hii inazingiatia idhini ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kuhusu Toleo hili la Hisa, na Wawekezaji ambao maombi yao yamekubaliwa wataingiziwa hisa zao katika akaunti zao zinazihifadhiwa na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE Central Securities Depository). Stakabadhi za Umilki wa Hisa zinaweza kupatikana kutoka kwa mawakala ambako Hisa husika zilinunuliwa.

Toleo la Hisa za Vodacom Tanzania limekuwa toleo kubwa zaidi na la kihistoria kufanyika nchini, na kuhusisha Watanzania zaidi ya 40,000 wengi wao wakiwa wanashiriki kwa mara ya kwanza katika masoko ya mitaji hapa nchini. Kwa hiyo, Toleo hili limewezesha kupanuka kwa ushiriki wa Wananchi katika soko la mitaji na dhamana, na pia katika uchumi wa Taifa.

Kwa kuzingatia ratiba iliyoidhinishwa, tarehe 7 Agosti 2017, ndiyo tarehe ya kutangaza matokeo ya toleo. Baada ya kuingizwa kwa hisa katika akaunti za CSD za Wanahisa, hisa zitaorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Saalam na mauzo yake kuanza saa 4 asubuhi, tarehe 15 Agosti, 2017. Wanahisa wanahimizwa kupata Stakabadhi za Hisa zao zilizohifadhiwa katika Hifadhi ya Dhamana (CSD) kutoka kwa Mawakala ambako walinunua hisa hizo.

Vodacom Tanzania inafurahi na kujivunia ukweli kwamba Watanzania wengi wamejitokeza kununua hisa zake. Aidha, Vodacom Tanzania inawashukuru wanahisa wote wa ndani na kutoka nje ya nchi kwa imani waliyoionyesha kwake na kuamua kuwa sehemu ya jamii pana inayounganishwa na maono ya kugusa maisha na kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidigitali.



This is the article MATOKEO YA UUZWAJI WA HISA 560,000,100 ZA VODACOM TANZANIA KATIKA SOKO LA AWALI "Credit News 24" this time, hopefully can benefit for you all. well, see you in other article post.

Title : MATOKEO YA UUZWAJI WA HISA 560,000,100 ZA VODACOM TANZANIA KATIKA SOKO LA AWALI "Credit News 24"
link : MATOKEO YA UUZWAJI WA HISA 560,000,100 ZA VODACOM TANZANIA KATIKA SOKO LA AWALI "Credit News 24"

0 Response to "MATOKEO YA UUZWAJI WA HISA 560,000,100 ZA VODACOM TANZANIA KATIKA SOKO LA AWALI "Credit News 24""

Post a Comment